Siri hizi zitafanya ndoa yako iwe ya kudumu na yenye furaha


- Kila mmoja wetu anataka kuwa na ndoa yenye ufanisi 'iliyoundwa mbinguni 'na kusawazishwa duniani.’ Siri za ndoa iliyo bora zimeibuka na ni kama zifuatazo: 

1. Kila mwanandoa ana dosari Read more 
Ni Mungu pekee aliyemkamilifu. Kila ua la waridi lina mwiba wake binafsi. Ukizingatia sana udhaifu wa mwenzako katika ndoa, hautafurahia wema wake. 

2. Kila utakaye oa ama kuolewa naye, ana siri kali
Hakuna aliye malaika, kwa hivyo koma kurejelea mambo ya zamani ya mwenzako.Kilicho muhimu ni maisha ya sasa ya mpenzi wako. Ya kale yamepita, jaribu kusamehe na kusahahu. 

3. Kila ndoa ina changamoto zake Ndoa si bustani la maua.Kila ndoa ya kuvutia imepitia jaribio lake la moto mkali.Mapenzi ya dhati hudhihirishwa wakati wa matatizo. 

4. Kila ndoa ina viwango tofauti vya ufanisi Usilinganishwe ndoa yako nay a mwingine yoyote. Hatuwezi kamwe kuwa sawa, wengine watakuwa mbele kabisa huku wengine wakiwa nyuma. Tia bidii, kuwa mvumilivu na baada ya muda ndoto kuhusu ndoa yako itakamilika. Kuoa ni kutangaza vita Unapoingia katika ndoa, ni sharti utangaze vita dhidi ya maadui wa ndoa baadhi yao ikiwa mapuuza, kukosa kusali, kutosamehe, usherati, uvivu, na kadhalika.Uwe tayari kupigana vita ili kudumisha ndoa yako 

5. Mungu hawezi kukupa mtu mkamilifu unayetamani Mungu hukupa kwa mfano wa malighafi ili kuunda unachotamani.Unaweza tamani mwanamke anayeoomba kwa saa moja ilhali mkeo huomba kwa dakika 30.Anaweza kuimarika kupitia mapenzi yako, maombi na kumtia moyo. 

6. Kuoa ni kujihatarisha  
Huwezi ukatabiri ni kipi kitatokea baada ya kufunga ndoa maadamu hali yaweza kubadilika kwa hivyo uwe tayari kwa lolote.Mnaweza kukosa mtoto kwa miaka mingine mine, huenda ulimwoa kutokana na umbo lake ndogo lakini akaongeza baada ya kuzaa.Huenda akapoteza kazi yake nzuri na ukalazimika kumudu familia kifedha hadi atakapopata kazi nyingine.mola akiwa nawe utatabasamu hatimaye. 

7. kila ndoa ina gharama ya kulipwa Ndoa ni kama akaunti ya benki.Ni zile pesa tu ulizoweka akiba katika benki unazoweza kutoa baadaye.Iwapo hautaweka akiba mapenzi, amani katika ndoa yako hautafurahia jamii yenye furaha.Huwezi kupenda pasipo kujitoa mhanga. Mola akupe neema na busara ya kuunda ndoa ya Mbinguni Duniani.  

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kunyonya Kyuma

Jinsi Ya kunyonya Kyuma Mpaka mwanamke apagawe!

HIZI NDIO SABABU ZINAZOWAFANYA WANAWAKE WENGI WATAMANI KUOLEWA NA MWANAUME MPOLE