Njia ya kupanga uzazi kwa kutumia Kalenda/ Kuzuia Mimba Kwa Njia ya Kalenda

Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia

 dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za 


kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha

 mwanamke. 
Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  

Nani anaweza kutumia njia ya kalenda

Moja, Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo.

Pili, Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake 

haubadiliki.

Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana. 

Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke

 kuandaa kalenda 

inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi 

kwa 

kipindi

 cha miezi 3 hadi 6.  Hii itamsaidia kujua lini mayai yake yalipevuka.  


Njia hii


 inamsaidia zaidi mwanamke aliye na mzunguko wa hedhi wa siku 28, na

 hutegemea kufahamu kuwa yai la mwanamke hupevuka siku 14 kabla hajaingina

 kwenye hedhi. 



Kwa mfano;

1. Kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 1 Juni (na una mzunguko wa hedhi 


wa siku 28), basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha 

hedhi tarehe 29 Juni.  Kwa hiyo yai lako litapevuka siku 14 kabla kwenye tarehe 15

 Juni.  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama

 unafanya mapenzi karibu na tarehe hii, kuanzia tarehe 14 Juni hadi 16 Juni.  

Kwa 


hiyo kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Lakini

 lazima ukumbuke kuwa mbegu za kiume zinaweza kuishi ndani ya mwili wa

 mwanamke kwa siku 7, kwa hiyo ili kuwa na uhakika Zaidi ya kuepukana na 

kupata mimba, una takiwa kutokufanya mapenzi kuanzia tarehe 8 hadi 16 Juni.



2. Katika mfano mwingine, kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 13 Juni (na 

una mzunguko wa hedhi wa siku 28), basi kuna uwezekano mkubwa utaingia

kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 11 Julai.  Kwa hiyo yai lako litapevuka siku 



14 kabla kwenye tarehe 28 Juni.  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako 


wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 27 Juni na 29 Juni.

  Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa

 usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 21 hadi 29 Juni. 

3. Katika mfano mwingine, kama baada ya kuandaa kalenda kuonesha mzunguko

 wako wa hedhi wa miezi 3 hadi 6 iliyopita, unagundua kuwa mzunguko wako ni 


wa siku 33 badala ya siku 28, basi kifuatacho ni kweli:  kama unaanza kuingia 

katika hedhi tarehe 1 Juni basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi

 kipya cha hedhi tarehe 4 Julai.  Kwa hiyo yai lako litapevuka kwenye tarehe 20

 Juni (Siku 14 kabla ya  tarehe 4 Julai).  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa 


kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 19 na 21 Juni.


 Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa

 usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 13 hadi 21 Juni. 

4. Katika mfano mwingine, kama baada ya kuandaa kalenda kuonesha mzunguko 

wako wa hedhi wa miezi 3 hadi 6 iliyopita, unagundua kuwa mzunguko wako ni 

wa siku 26 badala ya siku 28, basi kifuatacho ni kweli:  kama unaanza kuingia 

katika hedhi tarehe 1 Juni basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi

 kipya cha hedhi tarehe 27 Juni.  Kwa hiyo yai lako kitapevuka kwenye tarehe 13 

Juni (Siku 14 kabla ya  tarehe 27 Juni).  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa 

kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 12 na 14 Juni.

  Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa

 usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 6 hadi 14 Juni.



Faida ya kutumia njia hiyo


MOJA, Haina madhara yeyote ya kimwili.
Matatizo yanayoweza kujitokeza

MOJA, Njia ya kalenda si kinga dhidi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa 


mengine ya zinaa.


PILI, Njia hii ni ngumu na inahitaji wanawake kuwa wastadi katika hisabati, na

 kuwa waangalifu sana kuandika au kukumbuka tarehe ya kuanza kipindi chao 

cha hedhi cha mwisho.

TATU, Huchukua muda mrefu (miezi 3 hadi 6) kufahamu urefu wa mzunguko 

cha hedhi.

TATU, Mzunguko wa hedhi huweza kubadilika wakati wowote kufuatana na 

mabadiliko katika mwili.  Hii huweza kusababisha tarehe ya yai kupevuka kuwahi

 au kuchelewa, kwa hiyo mwanamke huweza kujiweka katika hatari ya kupata 

mimba bila kufahamu.



NNE, Ili njia hii iwe na uhakika, mwanamke hawezi kufanya mapenzi katika siku 

zake 9 kila mwezi ambapo kuna uwezekano wa yeye kupata mimba.  Kwa hiyo njia

 hii inahitaji uwezo mkubwa wa kujidhibiti na hufanya kazi vizuri iwapo 

mwanaume namwanamke wamekubaliana kufanya hivyo kwa pamoja, na 

mwanaume anamsaidia mwanamke kuhesabu au kuandika urefu wa mzunguko

 wake wa hedhi.

 TANO, Kwa sababu urefu wa mzunguko wa hedhi wa mwanamke huweza

 kubadilika ghafla bila kutegemea, hata kama inatumika inavyotakiwa, njia hii si 

nzuri kama njia nyingine zilizotajwa kuzuia mimba na kupanga uzazi.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI NDIO SABABU ZINAZOWAFANYA WANAWAKE WENGI WATAMANI KUOLEWA NA MWANAUME MPOLE

Jinsi ya kunyonya Kyuma

Jinsi Ya kunyonya Kyuma Mpaka mwanamke apagawe!