JINSI YA KUTUMIA KONDOM ZA KIUME


NUSU ya watu wanaotumia kondomu kwa ajili ya kujikinga na mimba ama magonjwa ya zinaa, hawajui namna ya kuitumia mipira hiyo





Tumia kondom mpya kila mara unapofanya mapenzi.
Jitahidi kutokugusa sehemu za siri ya mpenzi wako (au osha mikono yako) kabla ya kugusa sehemu zako za siri.

1. Usiguse sehemu za siri za mpenzi wako kabla ya kuvaa kondom. Angalia kwa makini paketi za kondom kabla ya kuifungua.
Hakikisha haijaharibika au kupasuka. 





Angalia tarehe ya mwisho ya matumizi ya kondom hii, ambayo itakuwa imechapishwa sehemu ya nje ya paketi ya kondom kuhakikisha tarehe haijafika. Kama tarehe imeishafika na kupita, tumia kondom nyingine. 


2. Fungua paketi kwa uangalifu kwenye sehemu iliyo na makucha makucha kama msumeno, ili kuhakikisha hauharibu kondom.
Usitumie makucha au meno kufungua paketi, kwa sababu kondom inaweza kuchanika.

Upapogusa kondom, iwe na utelezi kidogo. Kama kondom haina utelezi, imeharibika, kwa hiyo usiitumie. Sehemu ya nje ya kondom huwa na majimaji yanayorahisisha kufanya mapenzi. Kabla ya kuvaa kondom kwenye uume, hakikisha unafahamu sehemu gani inakaa nje unapoikunjua.

Tumia kondom mpya kila mara unapofanya mapenzi.
Usitumie tena kondom iliyokwisha tumika.


3. Weka kondom kwenye uume uliyosimama tu. Minya chuchu iliopo sehemu ya juu ya kondom kuhakikisha hamna hewa ndani yake. Hii ni kuhakikisha kuna nafasi ya kutosha katika kondom wakati mwanaume anamwaga shahawa.


4. Endelea kuminya chuchu na kunjua kondom kwa uangalifu hadi unapofika sehemu ya chini ya uume. Kuminya chuchu kunahakikisha kuna nafasi ya kutosha kupokea shahawa itakayomwagika.
Kama unaweka kondom juu ya uume na unaanza kuikunjua vibaya, usiitumie tena, kwa sababu ukiigeuza kuna uwezekano kuna tone chache za shahawa zilizokaa nje ya kondom.

Usitumie Vaseline, losheni au aina nyingine yeyote ya mafuta kuongeza utelezi wa kondom zaidi. Mafuta ya aina hii huongeza uwezekano wa kondom kupasuka. Kama unahitaji utelezi zaidi, tumia mate au majimaji maalum yaitwayo KY-Jelly, yanayopatikana katika duka ya madawa.

5. Anza kufanya mapenzi

6. Mara tu baada ya kufikia mshindo, toa uume ukeni wakati unaendelea kushikilia kondom kwenye sehemu ya chini ya uume karibu na mapumbu. Kila mara ondoa uume kabla haujalegea kuhakikisha kondom haiachii na kubaki ndani ya uke.

7. Kwa uangalifu, vua kondom kutoka kwenye uume

8. Funga kondom kwa fundo kwenye sehemu ile ya wazi kuzuia shahawa kumwagika.

9. Funga kondom kwenye karatasi au kwenye paketi yake ya mwanzo.

10. Tupa kondom kwenye choo cha shimo, au ichome moto. Nawa mikono yako na maji na sabuni.


Comments

Popular posts from this blog

HIZI NDIO SABABU ZINAZOWAFANYA WANAWAKE WENGI WATAMANI KUOLEWA NA MWANAUME MPOLE

Jinsi ya kunyonya Kyuma

Jinsi Ya kunyonya Kyuma Mpaka mwanamke apagawe!